George Opong Weah ahaidi kuwatumikia raia wa liberia
Akihutubia
baada ya kula kiapo, Bw Weah amesema: "Nimekuwa katika viwanja vingi
maishani, lakini sijawahi kuhisi hivi."Ameahidi kujitolea kuwatumikia raia
wa nchi hiyo.
"Nitafanya
zaidi ya mchango ninaotarajiwa kutoa ili kutimiza matarajio yenu - lakini
naomba nanyi mtimize matarajio yangu, siwezi kutimiza haya peke yangu."
Weah
alicheza mpira wa miguu katika klabu kadha za Ufaransa na Uingereza miaka ya
1980 na 1990 na akaibuka Mwafrika wa kwanza kushinda tuzo ya Fifa ya Mchezaji
bora wa mwaka duniani na tuzo ya Ballon d'Or.
Aligombea
urais mwaka 2005, na alimshinda Bi Johnson Sirleaf wakati wa duru ya kwanza
katika uchaguzi huo lakini akashindwa katika duru ya pili ambapo kambi yake
ilisusia kushiriki katika duru ya pili.


No comments