Kesi ya scopion ahukumiwa miaka 7 jela na faili milioni 30
Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam
imemhukumu, Salum Njwete maarufu Scorpion miaka 7 jela kwa kosa la kumjeruhi na
kumtoboa macho kinyozi, Said Mrisho, pia mahakama imemtaka kulipa faini ya TSH.
Milioni 30 kwa ajili ya fidia kwa majeruhi huyo.
Kwa upande wake, mlalamikaji katika kesi hiyo ambaye ni
majeruhi, Said Mrisho amelia mahakamani hapo akidai adhabu aliyopewa Scorpion
haitoshi ikilinganishwa na kosa alilotenda huku akieleza kuwa atakwenda kwa
Rais Dkt. John Magufuli kumueleza masikitiko yake.
Njwete anlikuwa
akikabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni unyang’anyi wa kutumia silaha na
kumjeruhi Said Mrisho kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali za mwili zikiwemo,
tumboni na mabegani na kisha kumtoboa macho kitendo anachodaiwa kutenda Septemba
6, mwaka jana katika eneo la Buguruni Sheli, jijini Dar es Salaam. Pia,
anadaiwa kumwibia mali yenye thamani ya Sh 476,000/-

No comments