Humphrey Polepole akataa kitu UKAWA Tanzania
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM),
Humphrey Polepole amesema kuwa hakuna kitu kinaitwa UKAWA kwani mpango huo
ulianzishwa na CHADEMA ili kuvitumia vyama vingine kisiasa.
Polepole amesema kuwa kama UKAWA ingelikuwepo hadi leo basi isingetokea
baadhi ya majimbo CHADEMA kushindana na CUF ile hali vyama vyote vipo chini ya
muavuli wa UKAWA.
“Hakuna kitu
kinaitwa UKAWA, hii ilikuwa project ya Chadema ikivitumia vyama vingine, CUF,
NCCR na NLD. Kilichobaki ni UKIWA, katika jimbo lililokuwa la CUF leo CDM na
CUF wanamenyana,”ameandika Humphrey Polepole kupitia Twitter.
Hata hivyo,
kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kinondoni CUF kwa upande wa
Prof Lipumba imesimamisha mgombea wake huku CHADEMA nao wakisimamisha mgombea
wao

No comments