Mwanafunzi Abdul Nondo apatikana
Miongoni mwa stori kubwa Leo March 7, 2018 ni
kuhusu taarifa za kutoonekana kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania,
Abdul Nondo ambae pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam ambaye ilidaiwa
kapotea katika mazingira ya kutatanisha jana usiku majira ya saa 5 hadi 6 na
kuacha ujumbe usemao “I AM AT HIGH RISK”
Mkurugenzi wa idara ya Sheria
ya Mtandao wa Wanafunzi Tanzania Paul Kisabo amesema kwamba Abdul Nondo
amepatikana mkoani Iringa katika wilaya ya Mafinga.
Nanukuu “Nondo amepatikana yupo mafinga
kituo cha polisi muda huu. Amezinduka jioni ya leo akiwa ametupwa, akauliza
watu kwamba yuko wapi wakamwambia yupo mafinga. Akajivuta kwenda kituo cha
polisi,” –
“Bahati nzuri alikuwa anakumbuka namba moja tu ya dada yake
akaomba simu polisi na kumpigia dada yake, Dada yake pia akamjulisha baba yake
mdogo wa huku dar tuliyekuwa nae leo” -Paul Kisabo
“Then
kupitia namba ya polisi kituo cha polisi Mafinga Nondo ameongea na baba yake
mdogo tuliyekuwa nae leo kupitia simu ya afande. Amenyang’anywa laini zake za
simu ila simu yake anayo. Ila yupo salama.” -Paul Kisabo

No comments